Sahani ya uji wa mtama.
Mtoto akipata uji, mchoro wa William Hemsley (1893).
Uji ni kinywaji kinachopikwa kwa kuchemsha unga na maji ukawa laini.
Mara nyingi hupendwa asubuhi na kwa ajili ya watoto na wagonjwa.
Unga unaotumika unaweza kuwa wa mahindi, lakini pia mtama, ulezi, uwele n.k.