Umaskini (kutoka neno la Kiarabu) ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile chakula, maji salama, huduma za afya, mavazi na nyumba kutokana na kukosa uwezo wa kuvinunua.[1] Hii pia inajulikana kama umaskini uliokithiri au ufukara.[2]
Umaskini wa kadiri ni kuwa na rasilimali chache zaidi au mapato madogo zaidi kulingana na watu wengine katika jamii au nchi au hali ya wastani duniani. Hali hii pia hujulikana kama umaskini halisi au unyonge. Umaskini linganishi ni hali ya kuwa na rasilimali chache au kipato cha chini kuliko wengine kwenye jamii au nchi, au ikilinganishwa na wastani duniani kote.
Umaskini unajumlisha pia matokeo yake upande wa siasa na jamii.[3]
Kupunguza ufukara ni kati ya malengo makuu ya taasisi nyingi za kimataifa, kama vile Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia. Benki hiyo imekadiria kuwa watu milioni 702.1 walikuwa wakiishi kifukara mno mwaka 2015, wakati walikuwa bilioni 1.75 mwaka 1990 (kutoka 37.1% hadi 9.6%).[4][5][6]
Kati yao, milioni 347.1 hivi walikuwa Afrika Kusini kwa Sahara (35.2% za wakazi) na 231.3 Asia Kusini (13.5%), lakini ufukara ni changamoto kwa nchi zote duniani.[7][8]
UNICEF imekadiria kwamba nusu ya watoto wote duniani wanaishi kifukara (bilioni 1.1).[9]
Wataalamu mbalimbali wamesema sera za uliberali mpya zinazofuatwa na taasisi za kiuchumi za kimataifa (kama vile IMF na Benki ya Dunia) zinazidisha tofauti za kiuchumi kati ya binadamu.[10]
{{cite encyclopedia}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite journal}}
: Unknown parameter |dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)