Umisionari

Umisionari ni utendaji unaolenga kueneza dini fulani, hasa zile zinazokusudiwa kuwa za kimataifa kutokana na misingi ya imani yake, kwamba ndivyo Mungu anavyotaka na alivyoagiza.

Asili ya neno hilo ni missio (kwa Kilatini utume).

Mmisionari au mwanamisheni ndiye mtu anayefanya kazi hiyo, hasa katika maeneo ambayo dini hiyo haipo au haijakua.

Mara nyingi wamisionari wanachangia pia maendeleo ya jamii, hasa kupitia elimu, utabibu, utunzaji wa watoto yatima na walioathiriwa na vita na maradhi mbalimbali.

Pengine uenezaji wa dini unatumia mbinu zisizokubalika kijamii, kama vile kulazimisha kwa namna moja au nyingine mtu asiyetumwa na moyo wake kukubali dini mpya.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne