Unyanyasaji wa kingono ni aina ya unyanyasaji unaohusisha matumizi ya matamshi ya ngono ya wazi au ya siri, ikiwa ni pamoja na ahadi zisizohitajika na zisizofaa za zawadi kwa kubadilishana na faida za ngono.[1]
Unyanyasaji wa kijinsia unajumuisha vitendo mbalimbali kama vile maneno yasiyofaa kwa jinsia nyingine. Unyanyasaji unaweza kutokea katika mazingira mbalimbali ya kijamii kama vile sehemu za kazi, nyumbani, shuleni, au kwenye taasisi za kidini.
Waathirika wanaweza kuwa wa jinsia yoyote[2], ingawa mara nyingi zaidi ni wanawake.