Upanga (kwa Kiing. sword) ni silaha yenye makali inayoshikwa mkononi kwa ajili ya kukata. Hutengenezwa kwa metali, hasa feleji, ikifanana na kisu ila tu ni kubwa. Hasa ubapa wake ni ndefu na mpini wake ni mkubwa kwa sababu mkono wote unahitaji kushika silaha hii.
Mara nyingi kuna chuma cha kupandana kinachokusudiwa kukinga mkono unaoshika upanga. Umbo la upanga ni muhimu kwa mbinu za mapigano.
Kuna aina nyingi za upanga zinazotofautiana hasa katika urefu na pia uzito.
Panga hutengezwa kutokana na malighafi ya shaba na chuma. Panga za kwanza zilitengenezwa na wahunzi (wafua chuma) wa Misri na China wakitumia bronzi. Tangu kupatikana kwa bunduki umuhimu wa upanga umepungua. Katika vita vya silaha za kisasa panga zimepotea kabisa. Lakini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe au ghasia ya Kenya ya mwaka 2008 panga zilikuwa silaha muhimu tena.
Upanga mwembamba huitwa kitara.