Upasuaji (kutoka kitenzi "kupasua": pia Operesheni kutoka Kiingereza "operation") ni matibabu maalumu yanayohusu tendo la kutibu mwili kwa kukata, na kurekebisha sehemu yenye maradhi au tatizo lingine lolote.
Mgonjwa ambaye anapasuliwa anaweza kuwa mtu au mnyama. Mpasuaji ni mtu ambaye hufanya upasuaji na mpasuaji msaidizi ni mtu ambaye husaidia katika operesheni.
Timu ya upasuaji huwa na mpasuaji, mpasuaji msaidizi, anayetia ganzi, muuguzi na fundi wa upasuaji.
Upasuaji wa kawaida huchukua muda wa dakika hadi saa kadhaa.