Usanisinuru

Kila jani kina kiwanda cha kikemia ndani yake.

Usanisinuru (pia usanidimwanga, ing. photosynthesis) ni mchakato wa kibiolojia na kikemia ambako mimea ya kijani inageuza nguvu ya nuru ya jua kuwa nishati ya kikemia. Inatengeneza kabohidrati ikitumia nguvu ya nuru ya jua na dioksidi kabonia ya hewani pamoja na maji.

Nje ya mimea kuna pia aina kadhaa za bakteria na hasa mwani zinazofanya usanisinuru.

Fomula yake ni

6 CO2 + 12 H2O + nuru → C6H12O6 + 6 O2 + 6 H2O
dioksidi kabonia + maji + nishati nuru → glukosi + oksijeni + maji

Usanisinuru ni msingi wa maisha yote duniani. Unajenga mada ogania ambayo ni chanzo cha lishe katika mtando chakula kwa karibu viumbehai vingine vyote kwa njia moja au nyingine. Kwa njia hii ni chanzo cha mtando chakula wa uhai wote.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne