Usher | |
---|---|
![]() Usher Raymond mnamo 2010
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Usher Raymond IV |
Amezaliwa | 14 Oktoba 1978 Dallas, Texas Marekani |
Asili yake | Chattanooga, Tennessee, Marekani Atlanta, Georgia Marekani |
Aina ya muziki | Pop na R&B |
Kazi yake | Mwimbaji Mtunzi wa nyimbo Mtayarishaji wa rekodi Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1994–hadi leo (anaimba) 1998–hadi leo(anaigiza) |
Studio | LaFace, Arista |
Tovuti | www.usherworld.com |
Usher Raymond IV (amezaliwa tar. 14 Oktoba 1978) ni mwimbaji wa R&B-pop, mtunzi wa nyimbo, na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Usher. Usher, alianza kujibebea umaarufu kuanzia miaka ya 1990 hivi. Tangu hapo, ameuza albamu zake takriban milioni 35 kwa hesabu ya dunia nzima na ameshinda Tuzo tano za Grammy.[1]
Mnamo tar. 13 Septemba ya mwaka wa 2008, Usher ameorodheshwa kwenye orodha ya Wasanii Wakali 100 wa Muda Wote na gazeti la Billboard.[2] Ni miongoni mwa wasanii wachache wa lika lake kuorodheshwa katika orodha hiyo. Usher ameanzisha studio yake mwenyewe, inaitwa US Records, na pia ni mmoja kati ya wamiliki wa mradi wa Cleveland Cavaliers.