Ushirikiano (wakati mwingine hujulikana kama umoja) ni mchakato wa makundi ya viumbe wanaofanya kazi pamoja kwa manufaa fulani, kinyume na kufanya kazi kwa ushindani kwa manufaa ya ubinafsi.
Aina nyingi za wanyama na mimea zinashirikiana kwa kiasi kikubwa, hasa katika suala la uhai; bila mimea asilimia kubwa ya wanyama tusingeweza kuishi, pia bila sisi wanyama asilimia kubwa ya mimea isingeweza kuishi.