Usimamizi (kutoka kitenzi kusimamia; kwa Kiingereza "management"[1]) katika biashara na katika shughuli ya kuwapanga binadamu ni kitendo cha kuwaweka watu pamoja ili kutimiza malengo na madhumuni yatakikanayo. Usimamizi unajumuisha mipango, kuandaa, kuajiri wafanyakazi, kuongoza na kudhibiti shirika (kundi la mtu mmoja au zaidi au wahusika) au juhudi kwa madhumuni ya kufanikisha lengo. Kugawanya rasilimali kunajumuisha kupelekwa na kutumika kwa rasilimali watu, fedha, teknolojia na maliasili.
Usimamizi unaweza pia kumrejelea mtu au watu wanaotenda tendo au matendo ya usimamizi.