Utamaduni

Michoro ya miambani huko Gobustan, Azerbaijan, 10000 KK ikionyesha utamaduni uliostawi.
Sanaa ya Misri ya kale, 1400 KK.
Dini na sanaa ni sehemu muhimu ya utamaduni wa binadamu.

Utamaduni ni jinsi binadamu anavyokabili maisha katika mazingira yake.[1] Hiyo inajumlisha ujuzi, imani, sanaa, maadili, sheria, desturi n.k. ambavyo mtu anajipatia kama mwanajamii.[2]

Kama sifa maalumu ya binadamu, inayomtofautisha na wanyama, utamaduni ni suala la msingi katika anthropolojia, ukihusisha yale yote yanayopokezwa katika jamii fulani, kama vile lugha inayounganisha watu wanaohusika nao, fasihi, mafungamano, ndoa, michezo, ibada, sayansi na teknolojia.[3]

Utamaduni ulioendelea unaitwa pia "ustaarabu".

Kila utamaduni unabadilikabadilika mfululizo: ndani ya watu husika, baadhi wanachangia na kuunga mkono mabadiliko, wakati wengine wanayakataa. Ujuzi mpya na teknolojia, pamoja na mahitaji ya uchumi, ni kati ya mambo yanayosukuma zaidi kubadili kiasi fulani utamaduni.

  1. "Meaning of "culture"". Cambridge English Dictionary. Iliwekwa mnamo Julai 26, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. James, Paul; with Magee, Liam; Scerri, Andy; Steger, Manfred B. (2015). Urban Sustainability in Theory and Practice: Circles of Sustainability. London: Routledge. uk. 53.
  3. Macionis, Gerber, John, Linda (2010). Sociology 7th Canadian Ed. Toronto, Ontario: Pearson Canada Inc. uk. 53.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne