Uwanja wa michezo wa Mutesa II ni uwanja wenye shughuli mbalimbali za kimichezo huko Kampala nchini Uganda. Hivi sasa hutumiwa zaidi katika mchezo wa mpira wa miguu (soka) na hutumika kama uwanja wa nyumbani wa kilabu ya Express F.C[1] inayoshiriki Ligi Kuu ya Uganda. Uwanja huu una uwezo wa kustahimili watu 20,200.[2] Uliitwa jina hilo kwa sababu ya jina la Mutesa II wa Buganda.