Uwanja wa michezo (Kilat. + Kiing.stadium) ni mahali pa mashindano ya michezo. Mara nyingi umezungukwa na majengo ambayo yanaweza kufunguliwa juu na kuwezesha umma kutazama onyesho hilo kwa kutumia nafasi za kusimama au kukaa. Viwanja mara nyingi hutumiwa pia kwa matamasha na mikutano ya hadhara.