Uwindaji (kwa Kiingereza hunting) ni desturi ya kuua au kukamata wanyama, hasa kwa ajili ya kujipatia chakula au kitoweo, lakini pengine kwa biashara, burudani tu, kama si kwa kukomesha wanyama waharibifu.
Mbali ya uwindaji halali, kuna ujangili unaohatarisha aina mbalimbali za wanyama kiasi cha kuwamaliza kabisa duniani.
Kama mnyama husika ni samaki, kazi hiyo inaitwa uvuvi.
Kabla ya kuanza uzalishaji, kwa karne nyingi binadamu wote walitegemea hasa uchumaji wa matunda na uwindaji.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uwindaji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |