Valle d'Aosta

Ngome ya Saint-Pierre, karne ya 13th,Valle d'Aosta
Mahali pa Valle d'Aosta katika Italia

Valle d'Aosta (kwa Kifaransa:Vallée d'Aoste; kwa Kiswahili: Bonde la Aosta) ni mkoa wenye kujitawala wa Italia. Ni mkoa mdogo kuliko yote kwa eneo (km² 3,263) na kwa idadi ya wakazi (126,935) na kwa sababu hiyo hauna wilaya ndani yake.

Mji mkuu wake ni Aosta.

Wakazi wengi wanaongea Kiitalia, lakini pia lahaja maalumu ya Kifaransa.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne