| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Inno e Marcia Pontificale (Kiitalia) Wimbo la Papa | |||||
Mji mkuu | Mji wa Vatikani1 | ||||
Mji mkubwa nchini | Mji wa Vatikani | ||||
Lugha rasmi | Kilatini2, Kiitalia | ||||
Serikali | Ufalme Papa Fransisko Pietro Parolin | ||||
Uhuru Mkataba wa Laterani |
11 Februari 1929 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
0.44 km² (ya 232) | ||||
Idadi ya watu - 2008 kadirio - Msongamano wa watu |
791 (ya 229) 1,780/km² (ya 6) | ||||
Fedha | Euro (€)4 (EUR )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .va | ||||
Kodi ya simu | +395
- |
Mji wa Vatikani ni dola-mji lenye eneo la kilomita za mraba 0,44 tu. Hivyo ni nchi ndogo kuliko zote duniani. Pande zote inazungukwa na Italia.
Idadi ya wakazi ni 791; raia ni 565 tu (mnamo Oktoba 2008).
Ni nchi ya Papa ambaye ni askofu wa Roma na mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote.
Jina limetokana na kilima cha Vatikani (kwa Kilatini: Mons Vaticanus) ndani ya jiji la Roma, upande wa magharibi wa mto Tiber.
Pamoja na Basilika la Mt. Petro, jengo la kanisa kubwa kuliko yote duniani, Vatikani ina makanisa mengine saba, jumba la Vatikani, ofisi za utawala wa Kanisa Katoliki, mabustani, stesheni ya treni, nyumba za kuishi, hosteli kwa ajili ya mafukara na makumbusho yenye hazina kubwa za sanaa kiasi kwamba nchi nzima inahesabiwa na UNESCO kuwa Urithi wa dunia (tangu mwaka 1984).