Verano wa Cavaillon (alifariki Cavaillon, Provence, Ufaransa, 590 hivi) alikuwa askofu wa mji huo maarufu kwa maadili yake, hasa huruma kwa wagonjwa[1].
Gregori wa Tours alisimulia baadhi ya miujiza yake.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kati ya watakatifu.