Vinsenti wa Paulo (Pouy, Gascony, 24 Aprili 1581 - Paris, 27 Septemba 1660) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki kutoka [[Ufaransa] maarufu hasa kwa huruma yake kwa maskini na kama mwanzilishi wa mashirika mawili ya kitawa.
Akiwa amejaa roho ya kichungaji, huko Paris alijitosa kuhudumia fukara, akitambua sura ya Bwana Yesu katika sura ya kila mtu mwenye mateso akaanzisha Shirika la Misheni, halafu, akishirikiana na Luisa wa Marillac, lile la Mabinti wa Upendo, ili kufufua maisha ya Kanisa la mwanzoni, kulea kitakatifu wakleri na kusaidia maskini[1].
Miaka 1605-1607 alikuwa mtumwa wa Waislamu, kwanza nchini Tunisia, halafu Uturuki.
Alitangazwa na Papa Benedikto XIII kuwa mwenye heri tarehe 13 Agosti 1729, halafu Papa Klementi XII akamtangaza mtakatifu tarehe 16 Juni 1737.