Vivina (pia: Wivina, Wivine; Oisy, leo nchini Ufaransa, 1103 hivi; karibu na Bruxelles, leo nchini Ubelgiji, 17 Desemba 1170) alikataa kuolewa akaishi kama mkaapweke hadi alipoanzisha monasteri akaiendesha kama abesi mpaka kifo chake[1][2].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Desemba[3]..