Waadventista Wasabato ni Wakristo Waadventisti wa madhehebu yanayosisitiza ujio wa pili wa Yesu yakisema uko jirani kutokea na kwamba utawahi wafuasi wake wakishika Sabato, si Jumapili.
Kati ya makundi yaliyoanzishwa Marekani baada ya utabiri wa William Miller kwamba ujio huo eti, utatokea tarehe 22 Oktoba 1844, lililoenea zaidi ni lile la Waadventista Wasabato (mwanzo rasmi mwaka 1863) ambalo kwa sasa lina waumini zaidi ya 17 milioni duniani kote.