Waadventisti

Kanisa la Waadventisti huko Jyväskylä, Finland.

Waadventisti ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali yanayosisitiza ujio wa pili wa Yesu yakisema uko jirani kutokea.

Ingawa sisitizo hilo lilijitokeza mara kadhaa katika historia ya Kanisa, lilipata nguvu mpya huko Marekani katika karne ya 19.

William Miller ndiye anayetajwa kama mwanzilishi wa tapo hilo kwa kufanya watu kati ya 50,000 na 100,000 kutarajia ujio huo utatokea tarehe 22 Oktoba 1844.

Baada ya siku hiyo kupita kama kawaida, wengi waliachana na utabiri huo, wengine walianzisha makundi mbalimbali. Miller hakujiunga na lolote, bali alihimiza umoja hadi kifo chake (1849).

Kati yake, lililoenea zaidi ni lile la Waadventista Wasabato (mwanzo rasmi mwaka 1863) ambalo kwa sasa lina waumini zaidi ya 17 milioni duniani kote.

Matawi ya Waadventisti yaliyotokea katika karne ya 19.

Mashahidi wa Yehova pia wana asili katika tapo hilo.

Jaribio la kutabiri tarehe ya ujio wa pili kwa kupiga hesabu kutokana na Biblia lilitokea tena na tena hadi karne ya 21 bila mafanikio.



From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne