Waanzilishi saba

Mtakatifu Aleksi Falconieri.

Waanzilishi saba wa Utawa wa Watumishi wa Maria, ni wanaume wa Firenze (Italia) ambao mwaka 1233 hivi waliacha shughuli zao wakaenda kuishi upwekeni ili kuanzisha shirika la maisha ya wakfu aina ya ombaomba kwa heshima ya Bikira Maria[1].

Majina yao ni: Buonfiglio wa Monaldi (Bonfilius), Yohane wa Buonagiunta (Bonajuncta), Amadeo wa Amidei (Bartolomeus), Rikovero wa Lippi-Ugguccioni (Ugo), Benedikto wa Antella (Manettus), Gerardino wa Sostegno (Sostene), na Aleksi Falconieri (Alexius), wa mwisho kufa (1310), ambaye ndiye maarufu zaidi.

Wote wanaheshimiwa katika Kanisa Katoliki kama watakatifu, na sikukuu yao ya pamoja huwa tarehe 17 Februari[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/26150
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne