Wakakwa

Rais Idi Amin mwaka 1973.

Wakakwa ni kabila la watu wanaoishi kaskazini magharibi mwa Uganda, kusini magharibi mwa Sudan Kusini na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Walitokea kaskazini (mji wa Kawa, leo nchini Sudan).

Lugha ya wengi wao ni Kikakwa (Kutuk na Kakwa), mojawapo kati ya lugha za Kiniloti na dini yao ni Uislamu.

Maarufu kati yao ni Idi Amin, dikteta wa Uganda miaka 1971-1979. Wakakwa na majirani wao Waaringa wanatuhumiwa kuwa walishirikiana naye katika maovu mengi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne