Wakonsesyoni

Ngao ya Shirika la Kukingiwa Dhambi ya Asili (O.I.C.).
Mtakatifu Beatriz.

Shirika la Kukingiwa Dhambi ya Asili (Ordo Inmaculatae Conceptionis), au Wakonsesyoni, ni shirika la wanawake wamonaki lililoanzishwa mwaka 1484 huko Toledo Hispania na Beatriz wa Silva (jina kamili kwa Kireno ni Beatriz de Menezes da Silva) (Campo Maior, Ureno[1] 1424 hivi – Toledo Hispania, 9 Agosti 1492).

Huyu mwanamke wa ukoo maarufu wa Ureno alijiunga na monasteri na hatimaye akawa mwanzilishi wa masista wamonaki wa shirika hilo.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira.

Njozi ya Bikira Maria kwa Mt. Beatriz wa Silva ambayo alimuagiza aanzishe shirikakwa heshima yake.

[2]

Mwaka 1484 Beatriz na wenzake kadhaa walitamalaki monasteri nyingine ya Toledo aliyopewa na malkia ili itumike kuheshimu Kukingiwa Dhambi ya Asili Bikira Maria.

Mwaka 1489, kwa ruhusa ya Papa Innocent VIII, walipokea sheria za Wasitoo,[2] wakiahidi kuadhimisha kila siku Breviari ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili, wakiwa chini ya askofu mkuu wa Jimbo kuu la Toledo.

Mwaka 1501 Papa Alexander VI aliunganisha jumuia hiyo na Wabenedikto lakini chini ya Kanuni ya Mt. Klara.

Mwaka 1511 Papa Julius II aliwapa kanuni mpya ya kwao, halafu kardinali Fransisko Quiñones aliwaandikia katiba maalumu.

Kuanzia mwaka 1507 shirika lilienea Ureno, Hispania, Italia, Ufaransa na Brazil.

Mwishoni mwa karne ya 20, kufuatana na utafiti wa Mercedes de Jesús Egido (19352004), shirika limeachana na athari ya muda mrefu ya Wafransisko.

Mwaka 1996 lilipewa katiba mpya inayosisitiza kufuata maadili ya Bikira Maria.

  1. Congregatio de Cultu Divino et Disciplina Sacramentorum (Kireno) - Decree from the Congregation for Divine Worship and the Discipline of the Sacraments (Vatican, 12 October 2010) which states that modern research has proven her birthplace to have been Campo Maior, in Portugal.
  2. 2.0 2.1 "Foley O.F.M., Leonard. "St. Beatrice of Silva", Saint of the Day, Lives, Lessons and Feast, (revised by Pat McCloskey, O.F.M.), Franciscan Media". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2014-09-03.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne