Walugbara ni kabila la watu wanaoishi kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kaskazini magharibi mwa Uganda, lakini pia kusini magharibi mwa Sudan Kusini.
Lugha ya wengi wao ni Kilugbara, mojawapo kati ya lugha za Kisudani[2] na dini yao ni Ukristo, lakini pia Uislamu.