Wamalila ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Mbeya Vijijini, kata za Isuto, Ilembo, Iwiji, Masoko, Santilya, Mapinduzi, Iwindi, Iyunga, vijiji vya Maganjo, Isangati, Jojo, Izumbwe, Inoro, Iswago na kwingine pia.
Lugha yao ni Kimalila, mojawapo ya lugha za Kibantu, ambayo inafanana sana na Kisafwa na Kinyiha kwa sarufi na maneno, na kutofautiana kwa baadhi ya matamshi na lafudhi.