Wamormoni

Kioo cha rangi kikionyesha njozi ya kwanza ya Joseph Smith.


Wamormoni ni kundi la watu wanaohusiana na dini ya Mormoni, iliyoanzishwa na Joseph Smith huko New York, Marekani, katika miaka ya 1820 akidai alipata njozi na kuonyeshwa kitabu kitakatifu.

Baada ya kifo chake (1844), Wamormoni walimfuata Brigham Young hadi eneo la Utah.

Leo wengi wao ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku ya Mwisho (kifupisho cha Kiingereza LDS Church).

Kiini cha utamaduni wao ni jimbo la Utah, ambapo wao ndio wengi kati ya wakazi wote, lakini siku hizi Wamormoni wanaoishi nchini Marekani ni wachache kuliko wanaoishi nje kutokana na umisionari mkubwa wanaoufanya duniani kote.

Idadi yao inakadiriwa kuwa milioni 15.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne