Washington, D.C.

Mji wa Washington, D.C.





Jiji la Washington

Bendera
Jiji la Washington is located in Marekani
Jiji la Washington
Jiji la Washington

Mahali pa mji wa Washington katika Marekani

Majiranukta: 38°54′36″N 77°0′36″W / 38.91000°N 77.01000°W / 38.91000; -77.01000
Nchi Marekani
Tovuti:  http://www.dc.gov/
kwa maana mbalimbali ya jina "Washington" tazama Washington (maana)
Nguzo ya Washington na Nyumba Nyeupe (White House)

Washington, D.C., rasmi inajulikana kama Wilaya ya Columbia na kwa kawaida huitwa Washington au D.C., ni mji mkuu na wilaya ya shirikisho ya Marekani. Jiji hili liko kwenye Mto Potomac, mkabala na Virginia, na linapakana na Maryland upande wa kaskazini na mashariki. Lilipewa jina la George Washington, rais wa kwanza wa Marekani. Wilaya hiyo imepewa jina la Columbia, mfano wa kike wa taifa.


Jina la mji mkuu limechaguliwa kwa heshima ya kiongozi wa uhuru na rais wa kwanza George Washington. Jina la "District of Colombia" likachaguliwa kwa heshima ya Kristoforo Kolumbus mpelelezi wa Amerika.

Mji wa Washington uko kando la mto Potomac kati ya majimbo ya Maryland na Virginia. Uko karibu na pwani la mashariki la Marekani. Hori ya Chesapeake ya Atlantiki iko 35 km kutoka mji. Anwani ya kijiografia ni 38°53'42"N na 77°2'12"W.

Washington D.C. ni tofauti na jimbo la Washington lililopo upande wa magahribi wa Marekani.

Hapa ni makao rasmi ya Bunge la Marekani, ya Rais pamoja na serikali yake na makao ya mahakama kuu. Kuna pia majengo ya kihistoria hata kama Marekani haina historia ndefu pamoja na makumbusho mazuri.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne