Waswahili ni jina la kutaja wakazi wa miji ya pwani ya Bahari Hindi katika Afrika ya Mashariki, hasa Tanzania na Kenya, ambao ni wasemaji asili wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya kwanza.
Neno "Swahili" linatokana na Kiarabu "سواحل" (sawahil) yaani pwani, kwa hiyo maana yake ni "watu wa pwani". Lakini wanaisimu wengine wanafikiri kwamba asili ya neno hili ni "siwa hili"[1].
Siyo makabila yote ya pwani ya Afrika ya Mashariki ambao ni Waswahili, k.m. Wamijikenda.
Kimbari ni Wabantu wakichanganyikiwa kiasi na watu wengine, hasa Waarabu, zamani pia Waajemi[2].
Kiutamaduni ni Waislamu wanaofuata madhhab ya Hanafi.
Pia ni kawaida kuwaita Waswahili wasemaji wa Kiswahili hata kama ni wa makabila mengine.
"Mswahili" ni pia namna ya kumtaja mtu mjanja kwa lugha ya mzaha.[3]