![]() | Makala haina vyanzo vya kutosha
Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote.
|
Watu wazima Kibiolojia linaweza kumaanisha watu wale walio hai, hasa wakiwa na afya njema, tofauti na wafu na wagonjwa. Lakini kwa kawaida linatumika kutofautisha wale waliofikisha umri au kuwa na uwezo wa kuzaa na watoto.
Kwa kwenda mbali zaidi, maneno hayo yanatofautisha waliokomaa kiutu na vijana pia ambao, ingawa wameshabalehe, hawana ukomavu ule unaohitajika kukabili majukumu yote katika jamii, hasa chini ya miaka 18[1].
Kwa msingi huo, sheria zinawapangia haki na wajibu kadiri ya nchi.
Kwa nchi kama Tanzania pengine utu uzima unahesabika kuanza miaka 40(Habari hii inatakiwa kuthibitishwa kwa kuonyesha vyanzo), wakati utoto ni kuanzia miaka 0 hadi 17 na ujana ni kuanzia miaka 18 mpaka miaka 40.