Waware walikuwa kabila la Tanzania walioongea lugha ya Kiware. Inaaminika kwamba lugha hiyo imekufa kabisa.
Takriban mwaka 1900 wasemaji wa Kiware waliishi kisiwani sehemu ya Mashariki ya Ziwa Viktoria.
Lugha yao labda ilifanana na lugha nyingine za Kibantu za majirani.
Haijulikani wanaongea lugha ipi siku hizi, wala kama wanaendelea kujiita Waware.