Sehemu ya | people |
---|---|
Native label | יהודים |
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihi | Kiebrania |
Dini | Uyahudi |
Ameitwa baada ya | Yuda |
Nchi | Israel |
Taifa alipo zaliwa | Yuda |
Studied in | Jewish studies |
Historia ya mada | Jewish history |
Mkabala na | Gentilitas |
Has list | lists of Jews |
Wayahudi (kwa Kiebrania יְהוּדִים, Yehudim) ni kundi la kikabila na la kidini lenye asili yake katika eneo la Israeli ya Kale (Mashariki ya Karibu). Kabila la Kiyahudi, taifa la Kiyahudi na dini ya Kiyahudi, yote yana uhusiano wa karibu sana, kwa sababu Uyahudi ndio dini ya jadi ya watu wa taifa la Kiyahudi
Katika utamaduni wa Kiyahudi, ukoo unarudi nyuma hadi kwa mababu wa Biblia kama vile Abrahamu, Isaka, Yakobo na wanae 12 katika milenia ya 2 KK. Lakini tangu kale wanaogeuka kuwa Wayahudi na kuingizwa ndani ya kundi lao, hadhi yao ni sawa na wale ambao wamezaliwa ndani ya kabila hilo.