Waziri Mkuu wa Tanzania ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anawakilisha serikali katika bunge la taifa. Yuko chini ya mamlaka ya rais.[1] Anateuliwa na rais akihitaji kuthebitishwa na wabunge wengi.[2]
Waziri Mkuu si kiongozi wa serikali lakini anaongoza vikao vya baraza la mawaziri wakati rais na makamu wa rais hawapo.[3]
- ↑ Katiba ya Tanzania, fungu 52: ana "ana madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za serikali; ...atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni; ...atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au
mambo yoyote ambayo Rais ataagiza "
- ↑ Katiba ya Tanzania, fungu 51 ""Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
atakayeteuliwa na Rais; ...uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge walio wengi."
- ↑ Katiba fungu 54,2