Wenzo

Kwa wenzo mtu anapandisha mzigo mkubwa

Wenzo ni mashine sahili inayosaidia kuhamisha na kupandisha mizigo mikubwa kwa kutumia nguvu ndogo.

Kimsingi ni pau kama gogo, mti au nondo inayowekwa chini ya mzigo kwa upande moja na kushikwa upande mwingine. Wenzo hulala juu sehemu ya mhimili inayoitwa "nukta fungwa" na nukta hii ni mahali pa kugeuza wenzo. Nukta fungwa inagawa wenzo kwa sehemu mbili zinazoitwa "mkono mzigo" na "mkono kani".

Utaratibu wa wenzo ni kimsingi ya kwamba kani ndogo kwenye mkono kani mrefu inapandisha mzigo mkubwa kwenye mkono mzigo mfupi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne