Whitney Houston | |
---|---|
![]() Whitney Houston akiimba kwenye Welcome Home Heroes with Whitney Houston mnamo 1991
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Whitney Elizabeth Houston |
Amezaliwa | Agosti 9 1963 Newark, New Jersey, US |
Asili yake | East Orange, New Jersey |
Amekufa | Februari 11, 2012 (umri 48) |
Kazi yake | Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mwigizaji, mtayarishaji wa rekodi, mtayarishaji wa filamu, mwanamitindo |
Ala | Sauti, piano |
Aina ya sauti | Mezzo-soprano[1] |
Miaka ya kazi | 1977–2012 |
Studio | Arista |
Tovuti | www.whitneyhouston.com |
Whitney Elizabeth Houston (9 Agosti 1963 - 11 Februari 2012) alikuwa mwimbaji maarufu, mcheza filamu na mwanamitindo kutoka nchini Marekani. Whitney ni mshindi wa Tuzo ya Grammy - akiwa kama mwimbaji bora wa pop/R&B, mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, mtunzi wa nyimbo na mwanamitindo wa zamani. Anafahamika zaidi kwa kuwa sauti kali yenye nguvu na mvuto.[2] Anafahamika zaidi kwa kupitia wimbo wake wa "I Will Always Love You" na "I Wanna Dance with Somebody" kutoka katika toleo lake la 'The Star Spangled Banner.'
Whitney ni mmoja kati ya wasanii wa kike waliopata mafanikio makubwa kabisa katika medani ya muziki. Moja kati ya albamu zake ambazo zilipata kuwa maarufu zaidi ni pamoja na The Bodyguard (Kibwagizo bora kwa mauzo bora kwa miaka yote) na ndiyo albamu yake iliyofanya vizuri kupita zote.
Whitney Houston alifariki mnamo tarehe 11 Februari 2012 katika mazingira ya utata. Mwili wake ulikutwa katika chumba cha hoteli ya Beverly Hilton huko Beverly Hills,California.[12]
{{cite book}}
: Cite has empty unknown parameter: |coauthors=
(help)