Wikipedia:Mwongozo (Kutaja vyanzo)

Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    

Vyanzo vya habari ni mahali tunapopata habari zetu za hakika. Katika Wikipedia vyanzo hivyo vinatakiwa kuonekana maana habari zisizo na vyanzo kuna uwezekano mkubwa wa kuondolewa.

Katika Wikipedia yetu mara nyingi si rahisi kuonyesha vyanzo kwa sababu wachangiaji wengi hawana nafasi ya kutumia maktaba nzuri zenye majarida na vitabu vya kitaalamu.

Kwa hiyo tunatumia mara nyingi vyanzo visivyo vya Kiswahili, na hasa vya Kiingereza. Ni sawa kunakili orodha ya vyanzo kutoka makala ya en:wikipedia. Kuna pia vyanzo vizuri vinavyopatikana mtandaoni.

Kumbuka: makala ya wikipedia si vyanzo vinavyokubalika! Lakini unaweza kutumia vyanzo vinavyotajwa katika makala za enwiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne