Wilaya ya Chato

Wilaya ya Chato ni wilaya mojawapo kati ya 6 za Mkoa wa Geita. Wilaya hii ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Biharamulo, mkoa wa Kagera, halafu mwaka 2012 ikasogezwa katika mkoa mpya wa Geita.

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 365,127 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 584,963 [2].

  1. [1]
  2. https://www.nbs.go.tz

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne