Wilaya ya Kiteto ni wilaya mojawapo kati ya 7 za Mkoa wa Manyara.
Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Kiteto ilihesabiwa kuwa 152,757[1], wakati wa sensa ya 2002 walikuwa 244,669 [2] . Idadi imeongezeka tena katika sensa ya mwaka 2022 walipohesabiwa 352,305 [3].
Kiteto imepakana na wilaya ya Simanjiro upande wa kaskazini, upanda wa mashariki na mkoa wa Tanga na upande wa kusini na magharibi na mkoa wa Dodoma.
Makao makuu ya wilaya yako mjini Kibaya.
Wenyeji ni hasa Wamasai.