Wilaya ya Maswa ni wilaya mojawapo kati ya 6 za Mkoa wa Simiyu.
Eneo la wilaya ni kilomita za mraba 3,398 na kati yake km2 2,375 zinafaa kwa kilimo, nyingine ni misitu na milima.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 344,125. [1] Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 427,864 [2].
Misimbo ya posta katika wilaya hii inaanza kwa 393...