Wilaya ya Mlele | |
Mahali pa Mlele katika Tanzania |
|
Majiranukta: 6°43′23″S 32°3′29″E / 6.72306°S 32.05806°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mkoa wa Katavi |
Wilaya | Mlele |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 118,818 |
Mlele ni wilaya mojawapo kati ya 5 za Katavi, ambavyo vyote vilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012. Awali maeneo yake yalikuwa sehemu ya wilaya ya Mpanda. Mwaka 2016 wilaya mpya ilimegwa ili kuanzisha wilaya ya Mpimbwe.
Makao makuu ya wilaya yako Inyonga.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 118,818 [1]. Wakati wa sensa ya mwaka 2012 idadi ya wakazi ilikuwa watu 282,568.