Wilaya ya Same ni wilaya mojawapo kati ya wilaya 7 za Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 269,807. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 300,303 [1].
Wilaya hii imepakana upande wa kazkazini na Wilaya ya Mwanga na nchi jirani ya Kenya, upande wa kusini na Mkoa wa Tanga na upande wa magharibi na Mkoa wa Manyara. Makao makuu yapo Same Mjini.
Upande wa kusini wa Milima ya Pare upo ndani ya wilaya pamoja na sehemu ya Hifadhi ya Mkomazi.[2]
Njia ya reli ya Usambara inapita wilayani.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)