Wilaya ya Handeni ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Tanga katika Tanzania.
Imepakana na wilaya ya Kilindi upande wa magharibi, wilaya ya Korogwe na Mkoa wa Kilimanjaro upande wa kaskazini, wilaya ya Pangani upande wa mashariki na Mkoa wa Pwani kwa kusini.
Mwaka 2002 ilikuwa na wakazi 249,572. [1] Iligawiwa katika Wilaya ya Handeni Mjini na Wilaya ya Handeni Vijijini mnamo mwaka 2012. Katika sensa ya mwaka 2022 waliobaki upande wa vijijini walihesabiwa 384,353 [2].