Wilaya ya Ifakara Mjini ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67500.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya ya Kilombero ilihesabiwa kuwa 407,880.[1] Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 290,424 waliobaki upande wa wilaya ya Ifakara Mjini, yalipokuwa makao makuu ya wilaya ya Kilombero, baada ya kuigawa na kuunda wilaya ya Mlimba [2].