Wilaya ya Kilolo ni wilaya mojawapo kati ya 5 za Mkoa wa Iringa, Tanzania, yenye Postikodi namba 51300.
Wilaya hii imepakana na mkoa wa Morogoro upande wa kaskazini na mashariki, wilaya ya Iringa Vijijini upande wa magharibi na wilaya ya Mufindi upande wa kusini.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 218,130[1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 263,559 [2].