Wilaya ya Kondoa ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Dodoma, Tanzania yenye postikodi namba 417000[1]. Makao ya halmashauri ya wilaya yapo Kondoa mjini.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Kondoa ilihesabiwa kuwa 269,704. Mnamo mwaka 2015 mji wa Kondoa umetengwa kuwa halmashauri ya pekee (Wilaya ya Kondoa Mjini). Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa waliobaki katika wilaya ya awali walihesabiwa 244,854 [2].
Ndani ya wilaya hii kuna Michoro ya Kondoa, mahali pa sanaa ya miambani ambayo ni mahali pa urithi wa dunia.