Wilaya ya Muleba

Mahali pa Muleba (kijani) katika mkoa wa Kagera.

Wilaya ya Muleba ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35500 [1].

Muleba ilikuwa tarafa ya Bukoba ikaanzishwa kama wilaya ya pekee mwaka 1984. Makao makuu yako kwenye mji wa Muleba uliokuwa na wakazi 10,000 wakati wa sensa 2002.

Wilaya ina tarafa tano za Muleba, Kimwani, Nshamba, Izigo na Kamachumu. Eneo la wilaya ni kilomita za mraba 3,444 pamoja na 7925 km² za maji ya Ziwa Viktoria zikiwa pamoja na visiwa 20.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne