Wilaya ya Sikonge ni mojawapo kati ya wilaya nane za Mkoa wa Tabora nchini Tanzania.
Wilaya ya Sikonge imepakana na wilaya ya Uyui upande wa kaskazini, upande wa kusini na mkoa wa Mbeya, upande wa magharibi na mkoa wa Rukwa, upande wa kaskazini-magharibi na wilaya ya Urambo na upande wa mashariki na mkoa wa Singida.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 179,883. [1] Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 335,686 [2].