Wilaya ya Tanganyika ni wilaya mojawapo kati ya 5 za Mkoa wa Katavi.
Hadi mwanzo wa mwaka 2016 wilaya hiyo ilijulikana kama "Wilaya ya Mpanda Vijijini" (Mpanda District Council). Jina jipya linatokana na Ziwa Tanganyika lililopo kwenye mpaka wa mashariki wa eneo hili[1].
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 179,136. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 371,836 [2].
Makao makuu ya wilaya yanajengwa katika kijiji cha Majalila kilichopo kwa sasa katika kata ya Tongwe. Uteuzi huu ulifuata sifa za Majalila kufikika kwa urahisi kutokana na kuwa kandokando ya barabara kuu Mpanda - Kigoma, kuwepo kwa matenki mawili ya maji, na kuwa katika mpango wa kunufaika na umeme wa REA (Wakala wa umeme vijijini)[3]