Wilaya ya Urambo

Mahali pa Urambo (kijani cheusi) katika mkoa wa Tabora kabla ya kumegwa.

Wilaya ya Urambo ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Tabora yenye postikodi namba 455.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 370,796 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 260,322 [2] baada ya maeneo ya magharibi kukatwa ili kuunda wilaya ya Kaliua.

Sehemu hii ilikuwa kiini cha utemi wa Urambo ambako mtemi Mirambo alijenga milki yake.

  1. [1]
  2. https://www.nbs.go.tz

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne