Wilaya ya Uyui

Mahali pa Uyui (kijani cheusi) katika mkoa wa Tabora.

Wilaya ya Uyui ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Tabora yenye postikodi namba 45200.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya hii ilikuwa na wakazi wapatao 396,623 waishio humo.[1] Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 562,588[2].

Makabila yanayopatikana huko ni Wanyamwezi, Wangindo, Wasukuma, Watutsi, Waha na Wanyiramba.

  1. Sensa ya 2012, Tabora Region - Uyui District Council
  2. https://www.nbs.go.tz

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne